Rais wa Kenya, William Ruto, amesema kuwa Mashindano ya Dunia ya Riadha “yanarudi nyumbani”, baada ya Nairobi kuchaguliwa kuandika historia kama jiji la kwanza barani Afrika kuandaa tukio hilo kubwa mwaka 2029.
“Ruto alisema ushindi huo ni ‘ushindi kwa vizazi vya wanariadha’ ambao wameifanya Kenya kuwa kinara wa ubora katika mbio za uwanjani na barabarani.
Jiji la Nairobi lilizishinda London ya Uingereza na Rome ya Italia katika kinyang’anyiro cha kupewa haki za kuandaa mashindano hayo, huku Munich ya Ujerumani ikichaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka 2031.
Baada ya kupoteza zabuni ya kuandaa Mashindano ya Dunia ya 2025 yaliyokwenda Tokyo, Kenya ilirejea kwa nguvu zaidi na safari hii ikafanikiwa kuzizidi nguvu nchi zake washindani kutoka Ulaya.
